GET /api/v0.1/hansard/entries/1236315/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1236315,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236315/?format=api",
"text_counter": 393,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": "uchunguzi thabiti ufanywe ili tujue kundi lake ambalo anafanya nalo kazi. Ni lazima pia tujue iwapo katika kuhujumu, ni watu gani ambao wanampa nguvu kuweza kufanya jambo hili pasi na kuwa na kigegezi na uoga. Ni lazima sasa tuangalie kuwa shughuli zetu za kidini zinaangaziwa, ama tuwe tunavidhibiti. Kwa Kiingereza, wanasema regularisation . Ni lazima tudhibiti mambo ya makanisa na nyumba za kidini ili tujue vidhibiti tutakavyoviweka ndio tujue shughuli zinazofanyika katika nyumba hizi za ibada. Tusiangalie tu itikadi kali katika mambo ya AlShabaab, bali tujue kuwa itikadi kali ziko katika nyanja zote. Hata sisi kule kwetu kuna wakati kulikuwa na Sheikh fulani aliyekuwa akiwaambia watu wasiende shuleni, wasisome na wakisoma watakuwa wanaenda kinyume cha dini. Kwa hivyo, jambo hili liko katika sehemu nyingi sana. Tufungue macho yetu sana na tuangalie sehemu nyingi katika mambo ya itikadi kali zinapatikana vipi na zinafanyika vipi. Hata katika taasisi zetu za masomo na vyuo vikuu, mambo haya yanafanyika na ndiyo tunakuwa na mambo mabaya kama haya. Ninasema pole sana kwa wale ambao wamepoteza familia zao kutokana na tukio hili. Lakini sasa vikosi maalum vipelekwe pale, kuwekwe fence na kuangaliwe kinaga ubaga ili ijulikane wale wote ambao wamepotea na ambao wamezikwa maiti zao zipatikane. Na wale ambao bado wako katika hali mbaya waweze kuokolewa ili waweze kurejesha uhai wao. Ninataka niseme Wakristo wanasema sio wote wanaomuita Bwana watauona ufalme wa mbinguni. Tuna wale ambao ni wachungaji lakini si wachungaji wa ukweli, ni mitume wa uongo. Kwa hivyo, lazima tuwe macho jameni."
}