GET /api/v0.1/hansard/entries/1236322/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1236322,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236322/?format=api",
    "text_counter": 400,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kinango, PAA",
    "speaker_title": "Hon. Gonzi Rai",
    "speaker": null,
    "content": " Asante, Mhe. Spika wa Muda. Ninaomba niungane na wenzangu kumushukuru Mhe. Owen Baya kwa kuleta Hoja hii. Lakini ningetaka kutofautiana na wenzangu kwa michango ambayo wameifanya hapa kwa sababu nchi yaomboleza na bado itaendelea kuomboleza. Msiba huu ulituanza mwaka wa 2003. Historia inatuambia kwamba ulipofika mwaka wa 2016, yuko ndugu anaitwa Mwachiru ambaye aliuza mali yake na akamkabidhi Mackenzie karibu Ksh20 milioni, akanunua kituo cha televisheni na kuanza kutangaza masuala yanayohusiana na itikadi ya dini yake. Na Serikali ilikuweko. Ninashangaa licha ya haya yote kutokea, Mackenzie bado hayuko ndani. Lakini Mackenzie hastahili kuwa ndani peke yake. Mwaka wa 2018, Dkt. Ezekiel Mutua alitoa taarifa kwa Serikali kufunga kituo hicho cha runinga kwa sababu ya ujumbe wa Mackenzie lakini Serikali iliweka pamba kwenye masikio. Na hata kama alishikwa, inaonekana alikuwa na mkono mrefu kushinda Serikali."
}