GET /api/v0.1/hansard/entries/1236323/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1236323,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236323/?format=api",
    "text_counter": 401,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kinango, PAA",
    "speaker_title": "Hon. Gonzi Rai",
    "speaker": null,
    "content": "Inaonekana Mackenzie aliununua uhuru wake. Ana stesheni ya redio na serikali yake, ndiyo maana ana uhuru wa kufanya yale anayoyataka katika nchi hii. Leo jamii zaomboleza kwa sababu wamepoteza wapendwa wao mikononi na machoni mwa Serikali. Hakika, kuna kitu fulani kinachokosa. Mackenzie amewahi kushikwa na kupelekwa kortini kisha akaachiliwa kwa dhamana. Mambo haya yalikuwa yashaanza kuonekana yakifanyika. Mpaka sasa bado tumefunga macho na kusema kwamba Mackenzie ni mtu wa kupelekwa mahakamani. Angekuwa ashapelekwa Uholanzi na kufunguliwa mashtaka. Katika mazungumzo yake, Mackenzie alisema idara ya upelelezi ifanye uchunguzi wa kutosha na waache kumnyanyasa kiasi cha kwamba anatafuta uhuru wake wakati ambapo taifa linaomboleza watu karibu 100. Bado amezungumza kwa nguvu kana kwamba ana imani kwamba kwa vyovyote vile, atafika kortini na kuambiwa ushahidi umekosa. Watu wamekufa na ushahidi unakosekana kwa sababu hakuwapiga bunduki. Kwamba, kuna mjumbe fulani anayehubiri kwa kutumia redio na kwa kutumia congregation na kuwaumiza watu kiasi hiki, lakini sheria ikakosa mwelekeo mpaka ikafika mahali leo, hata mahakama iliyomwachilia kuna kesi bado pending . Tena tunataka kufungua kesi nyingine. Hiyo pia ibaki kortini? Wale waendelee kuomboleza, Mackenzie aendelee kukaa kwa sababu… Kwa nini aliposhikwa hangeambiwa, “Hatutakupa chakula ukiwa hapa ili tukuone utafika wapi na kutokula. Si unataka kumwona Mungu? Tunakupeleka kwa Mungu haraka.” Tunampeleka kortini kufanya kazi gani? Wenzake amewapeleka mbinguni lakini yeye anataka kubaki hapa ardhini. Kufanya nini? Ni haki yake kule rumande pia aachishwe kula chakula aambiwe tunataka tumuone namna gani ataishi na pesa zile alizokuwa akipewa na raslimali alizozichukua. Aulizwe alikua anataka kuzipeleka wapi ili tujue haki imefanyika kuliko kumpeleka mahakamani na mwisho tuambiwe Paul Mackenzie amaeachiliwa kwa sababu ushahidi umekosekana! Amezuka mwingine huko Tongaren. Naye pia tunampapasa. Alisema watu wasulubiwe. Alipoambia asulubiwe yeye, alisema kunaumiza. Jamani, twataka dhibitisho la aina gani?"
}