GET /api/v0.1/hansard/entries/1236381/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1236381,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236381/?format=api",
    "text_counter": 50,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Mheshimiwa Spika, wiki iliyokwisha, tulikuwa katika Kaunti ya Kilifi nilipomzindikiza Sen. Mdazayo, kuhutubia Bunge lile. Makaribisho waliotupatia wawakilishi Bunge wa County ya Assembly ya Kilifi yalikuwa murwa sana. Leo nimewakaribisha katika Kamati ya Delegated Legislation ambao ndio wamezuru. Kusema ukweli, ni Wabunge na maafisa ambao wako tayari kusoma kutoka Bunge letu. Mheshimiwa Spika, ni masikitiko kwamba, kwa sasa, Kaunti ya Kilifi imegubikwa na msiba mkubwa kutokana vitendo vinanvyoendelea vya kanisa mbili ambazo zinahubiri sehemu hiyo. Tunawaombea Mungu wakaazi wa Kaunti ya Kilifi. Mungu awape subira na nguvu ya kupambana na vitendo vya makanisa kama hayo ambayo kwa hakika ni aibu katika nchi yetu ya Kenya katika karne hii ya 21."
}