GET /api/v0.1/hansard/entries/1236415/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1236415,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236415/?format=api",
"text_counter": 84,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Asante, Mheshimiwa Spika, kwa fursa hii ambayo umenipatia ili nichangiae Kauli iliyoletwa na Seneta wa Kaunti ya Mombasa, Sen. Faki, kuhusu barabara ya Jomvu kuelekea SGR. Mheshimiwa Spika, naifahamu barabara hiyo. Ni kweli kuwa barabara hiyo iko vibaya sana. Barabara hiyo ni muhimu kwa sababu inasaidia wasafiri kutoka Magongo na Jomvu kuelekea SGR. Barabara hiyo naifahamu vizuri kwa sababu nimekulia maeneo ya Magongo na ni ukweli kuwa inaumiza magari. Kwa hivyo, ningeomba Kamati ya Barabara na Usafiri, itie bidii na ilete Taarifa ya kutosha ambayo itaeleza ni kwa nini ile barabara imesitishwa kutengenezwa. Kando na hilo, Kamati hiyo iko na Taarifa niliyouliza kuhusu barabara mbili za Kaunti ya Taita Taveta, ambayo ni barabara ya Taveta kuelekea Njukini na Ilasiti. Miezi miwili imeisha na sijapata Taarifa ama habari kamili kuelezea ni kwa nini ile barabara ilisitishwa. Barabara ya pili ni ya Mghange kuelekea Werugha, Wundanyi, Mbale na Mti wa Magoti. Barabara hizo zote zimesitishwa. Ningependa nipate Taarifa kamili kutoka kwa Kamati ya Barabara na Usafiri ya Seneti ikielezea ni lini wanakandarasi watarudi kutengeneza barabara hizo. Asante, Mheshimiwa Spika."
}