GET /api/v0.1/hansard/entries/1236584/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1236584,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236584/?format=api",
"text_counter": 253,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Tumeona kuwa ni wengi ambao wanaanzisha dini hizi. Imekuwa rahisi sana katika nchi yetu ya Kenya. Mtu anenda kwa Registrar of Societies kuomba kibali kuanzisha dini yake. Anatoka hapo na cheti cha kuanzisha dini yake. Kuna wengine nia zao ni safi. Lakini wengi wao, tumekuja kuona ya kwamba wanaanzisha dini zao kwa sababu ya pesa. Hizi pesa zimeanza kupita mpaka zimeingilia wale tunaowaweka mbele ya madhabahu. Wameziweka mbele pesa sana mpaka zimekuwa kama shetani. Ni muhimu sheria mwafaka zizingatiwe. Tumeona katika eneo la Shakahola, watu wengi wamepoteza maisha yao. Wengi walioathirika ni watoto wachanga. Mimi ninakubali ya kwamba, kama kuna watu wanaopenda kula ni watoto wachanga. Hii ni kwa sabau mili yao iko na nguvu nyingi. Lakini wao ndio wengi wa waliofariki. Hii ni ushuhuda tosha ya yote yanayoendela kule hivi sasa. Wengine hawajafariki kutokana na njaa lakini wameadhiriwa kwa magongo ama silaha fulani na kupoteza maisha. Hoja hii ni muhimu sana. Tuna imani Maseneta ambao wamechaguliwa wanajuhudi na wanaweza kufanya kazi."
}