GET /api/v0.1/hansard/entries/1236586/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1236586,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236586/?format=api",
"text_counter": 255,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Watu kama sisi ambao tunatoka katika sehemu hiyo, imebidi tujiweke kando kwa sababu, tuko na uchungu sana. Kwa hivyo, tunaweza kukosa mwelekeo wa fikira, mawazo ama kujadiliana. Ndio sababu niliona nikae kando ili niangalia suala hili kisawasawa. Mimi nitalivalia njuga na kuona ya kwamba suluhisho imepatikana. Mara nyingi, kuna mzaha unaofanywa na wanaojiita wakuu wa dini. Tuliona wakati fulani katika runinga, wakiweka sindano kwenye vidole vyao na kugeuza maji yaliosawasawa ya kunywana kuwa damu. Na kwa sababu mtu ni mgonjwa na hana imani, anatiwa imani ya kwamba amepozwa kwa sababu ametolewa damu chafu na kubakishwa ile safi kwenye mwili. Hayo yote tumeyaona. Jopo kama hili letu ambalo tunataka kulifanya hapa liweze kuleta suluhu kwa mchezo kama huu. Jambo kama hili lisitendeke tena mahali popote katika jamii yetu. Tuemeona watu wengi wa dini wamekuwa matajiri na kujiuliza kama tithe ama sadaka, tunayotoa inaweza kumfanya mhubiri ama kasisi kuwa tajiri namna ile. Watu wameuza nyumba zao na mali zao ili kusaidia kanisa. Lakini wakati mwingine ni kwa sababu wametiwa ile imani na wala sio kwa mapenzi yao. Lazima kuwe na sheria mwafaka. Tuko na imani na jopo hili. Watakapoanza kazi ile, waje na sheria ambazo zitatusaidia. Jambo la mwisho, jopo hili halitafaulu ikiwa Serikali haitajibika. Mimi nina imani na Maseneta ambao wamechaguliwa katika jopo hili. Watakapoifanya kazi hii, wasiogope kutwambia ukweli. Ninajua katika furukuta nyingi, watapambana na vitu ambavyo pengine itabidi wasiseme. Tunawaambia ya kwamba wawe na moyo mshupavu na wasiogope lolote wakijua ya kwamba Bunge hili ndilo limewatuma kufanya kazi hiyo na litawatetea kikamilifu. Bw. Spika, mimi ninaunga mkono. Tuko na imani kwamba wote ambao wamechaguliwa watafanya kazi hii. Asante."
}