GET /api/v0.1/hansard/entries/1236626/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1236626,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236626/?format=api",
"text_counter": 295,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13200,
"legal_name": "Issa Juma Boy",
"slug": "issa-juma-boy"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii niweze kuchangia suala hili. Maafa ambayo yametokea hivi juzi kule Kilifi ni maafa ambayo yanasikitisha ulimwengu mzima. Runinga zote hapa nchini na ulimwanguni, hasa Cable NewsNetwork (CNN) na Aljazeera zinaangazia maafa yaliyotokea Kilifi. Inasikitisha sana. Mwenyezi Mungu aijalie nchi yetu iwe na amani na watu wawe watulivu kwa sababu imefika pahali ambapo maiti zinafufuliwa kila siku. Ninashangaa maiti hizi zilizikwa namna gani pale Shakahola. Bw. Spika, nina imani na Maseneta waliyochaguliwa katika Kamati hii ambayo itashughulikia suala hili. Nawaomba washughulike na kufuatilia ili tujue shida hii ilianza namna gani? Bw. Spika, sisi kama Wakenya na Maseneta tuna huzuni kwa sababu ya hili jambo ambalo limetokea. Ni lazima sisi kama Wakenya tuombe ili nchi yetu iwe na amani. Haya makanisa yanastahili kujitakasa na yaje pamoja ili tuweze kutatua hili jambo kama Wakenya. Bw. Spika, sitaki kusema mengi kwa sababu nikifanya hivyo, tutatalizana bure hapa. Jana niliposikia kwamba maiti zilizofufuliwa zimefika 103, nilimaka muno. Sisi wenyewe lazima tuambiwe hivi leo vile maiti 103 zilipatikana Shakahola. Aaiigh! Bw. Spika, hata sina la kusema isipokuwa lililobaki ni kumwomba Mwenyezi Mungu ili ukweli upatikane Asante, Bw. Spika."
}