GET /api/v0.1/hansard/entries/1236647/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1236647,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236647/?format=api",
"text_counter": 316,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "kumechanganywa watu walio na uzoefu mkubwa na watu kutoka dini tofauti, ikiwemo Wakristo na Waislamu. Ninajua hii kazi ambayo wanaenda kufanya si rahisi. Kazi ya kujaribu kung’amua ukweli wa matukio ya maeneo ya Kaunti ya Kilifi, katika maeneo ya Shakahola na matukio ambayo yamepelekea vifo vya watu zaidi ya 95. Nikiangalia hizi hoja ambazo zimeangaziwa hapa, inatakikana tupanue majukumu ama mandate ya hii Kamati. Hii ni kwa sababu, kuna uchunguzi ambao unatakiwa kufanywa ili kuangazia majukumu ya asasi za kiusalama na vyombo vya dola, kuangazia yale mambo ambayo walifanya ama walifaa kufanya na hawakufanya. Tuko na kitengo cha ujasusi, polisi na idara ya uchunguzi. Ilikuwaje kwamba yote hayo yalitokea, bila asasi za usalama kungundua? Kwa hivyo, majukumu ya hii Kamati yaongezwe ili kuangalia yale mambo ambayo yangefanywa na asasi za usalama na dola za kitaifa. Walifanya mambo gani na ni gani hawakufanya? Bi Spika wa Muda, la mwisho ni kwamba hii kazi ambayo wanaenda kufanya ni ngumu. Ninasema hivi kwa sababu kuna ibara ya 32 ambayo inaangazia uhuru wa kuabudu kwa wananchi na pia uhuru wa kidini. Kwa hivyo, ninajua kutakuwa na mapendekezo mazuri ambayo yatasaidia kunyoosha barabara ya kuhudumu, ama kuangazia masuala ya kuabudu katika nchi yetu. Ninashukuru kwa hii Hoja na tutangojea mapendekezo ya Kamati ili tuangalie vile tutatengeneza kanuni za kusaidia kuendeleza mambo ya dini Kenya."
}