GET /api/v0.1/hansard/entries/1236656/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1236656,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236656/?format=api",
    "text_counter": 325,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Nachukua fursa hii kuunga mkono Hoja hii na Kamati iliyoteuliwa. Hawa ni watu ambao wana uwezo na ujuzi wa kutekeleza haya majukumu. Kwanza, ijulikane wazi ya kwamba jukumu hili tunalowapa kama Seneti sio jukumu ndogo. Ni nzito. Nimemsikiza Sen. Mungatana, MGH, na tayari amekubali. Anajua ni jukumu nzito na wataenda kukabiliana na majukumu mazito. Nikijaribu kulinganisha, wataenda kukabiliana na mazini yenyewe. Bi. Spika wa Muda, ukikumbuka wakati Seneta alienda kuangalia mambo ya Jim Jones, ilifika wakati fulani Seneta huyo akauwao. Kwa hivyo, hata hawa Maseneta wetu, tunawaambia majukumu ambayo mtapambana nayo ni magumu. Hata hivyo, najua mko tayari na mumeyavalia njuga ili muweze kukabiliana na kufikia kitovu chake. Nyinyi ni tegemeo letu. Bi. Spika wa Muda, katika riwaya ya Kisima cha Giningi, mhusika mkuu husema anapofika kanisani, hawaoni waumini kama waumini, bali kama customers au wateja"
}