GET /api/v0.1/hansard/entries/1236658/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1236658,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236658/?format=api",
    "text_counter": 327,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "wake. Pia hapa nchini nalinganisha mhubiri fulani na hali hiyo. Ulafi ambao unaonekana katika nchi yetu unapata wahubiri wengi hawaoni waumini kanisani, bali wateja wao. Ninamuona Sen. Wafula yuko katika Kamati hii. Ninawaomba mliangazie suala hili kwa undani kabisa. Tuangalie vizuri tuone ni kwa nini maafa haya yalitokea? Je, ni umaskini tulio nao katika nchi ya Kenya ambapo waumini wanaenda wanafunzwa mambo ambayo hayafai? Sio wachungaji peke yao wana makosa, hata sisi kama waumini tuna makosa kwa sababu tunapaswa kung’ang’amua ni lipi mbivu na ni lipi mbichi. Nilikuwa naangalia jambo fulani katika simu yangu na nikaona watu wamepiga foleni ili waongezewe nguvu za kiume. Niliogopa na nikashindwa la kusema. Tukio hili halikufanyika katika hospitali. Baada ya hapo, wanaambiwa kutoa sadaka. Ni vizuri Kamati hii iangazie mambo haya yote kwa undani sana. Bi. Spika wa Muda, nampongeza Askofu wa Kanisa la Katoliki la Nyeri ambaye alisema atakuwa katika msatari wa mbele ili utajiri wake au hela alizo nazo zichunguzwe. Hii ni kwa sababu utajiri ndio unaleta changamoto katika nchi yetu ya Kenya watu wakijaribu kuleta umaarufu wa hela pamoja na umaarufu wa---"
}