GET /api/v0.1/hansard/entries/1236701/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1236701,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236701/?format=api",
    "text_counter": 370,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante sana Bi. Spika wa Muda kwa nafasi hii. Kwanza ni kushukuru Seneta wa Kakamega, Sen. (Dr.) Khalwale, kwa kuleta Hoja hii kwenye Seneti, ili mambo ya kiroho vile vile yaweze kujadiliwa kwa akili na kudhibitiwa kimwili. Katika vyombo vya habari na mashinani tunakotoka, tunaona maajabu na vituko. Kwa mfano, unapata mhudumu wa injili akiwarai wafuasi wake, wainue marinda ama watoe mishipi na kugusagusa sehemu zao za “transformer”, na kuwapa matumaini kwamba watapata uponyaji ama watoto. Kuna wale ambao wanaambiwa watoe mashati na unamuona muhudumu anagusagusa matiti huku akicheka akikejeli akisema, “wewe hauogopi televisheni?” Lazima wananchi wa Kenya wapate haki. Injili inahubiriwa kwa ukweli. Uongozi wa makanisa lazima uwe kielelezo kwa jamii, kwa tabia na matamshi. Kuna vituko unapoona televisheni unashangaa. Tuko katika kipindi cha vioja mahakamani ama kukuza nyoyo za wakristo tukitarajia urejeo wa Kristo yesu. Kwa niaba yangu, watu wa Bungoma na Seneti, tutafanya kazi hii kwa uadilifu. Tutawapa washika dau wote nafasi kujieleza. Muungano wa kanisa wako na nafasi wajieleze, waalimu ambao hufunza watoto wale shuleni, ambao wanawaeleza waalimu mambo mengi wajieleze. Vyombo vya dola vile vile watueleze. Lakini, msimamo ambao tutatoa kama Seneti, lazima Serikali iwe tayari kutekeleza mapendekezo yetu. Hii ni kwa sababu, ninajua wengi waliapa kutetea baadhi ya wale ambao tunashtumu leo na wataogopa ya kwamba iwapo watashtumu huenda upako ambao waliahidiwa hautarudi tena. Sitaki kupita hapa, ila nakushukuru na kuahidi watu wa Kenya kwamba tutafanya kazi kwa uwazi, ukakamavu, upole na uajibikaji, ili Wakenya wasiporwe, wasipunjwe, wasihadaiwe wala kudanganywa, ili wawe na uwezo wa kuamua njia watakayo---"
}