GET /api/v0.1/hansard/entries/1236734/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1236734,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236734/?format=api",
"text_counter": 403,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "ama the Equalization Fund Appropriation Bill. Ningefurahia kuongezea sauti ya watu wa Kaunti ya Taita-Taveta kuandamana na maoni yao juu ya Mswada huu. Kabla sijaendelea, ningependa kusema ya kwamba, ninaungana na Maseneta wachache, akiwemo, Senata wa Kaunti ya Makueni, Sen. Maanzo, kwa kuupinga Mswada huu kwa sababu Mswada huu unaendelea kubagua magatuzi tofauti tofauti nchini Kenya. Watu wa Kaunti ya Taita-Taveta, waliunga mkono Katiba hii kwa sababu ilileta usawa wa ugavi wa raslimali kupitia njia mbili. Njia ya kwanza ilikuwa na ugatuzi na ulihakikisha ya kwamba fedha zinatoka katikati ama Nairobi na zikienda kwa magatuzi."
}