GET /api/v0.1/hansard/entries/1236736/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1236736,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236736/?format=api",
"text_counter": 405,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Njia ya pili ambayo ilinuiwa kuhakikisha ya kwamba maendeleo yameenea kila mahali nchini na kuleta usawa katika magatuzi ambayo yaliwachwa kimaendeleo ilikuwa ni Ibara 204 ambayo ilileta fedha ama mgao wa usawazishaji katika magatuzi tofauti tofauti ya Kenya. Wakati tulipata uhuru, kulikuwa na ile sera ambayo iliitwa Sessional Paper No.10 ya mwaka wa 1965 ambayo ililetwa katika Baraza la Mawaziri na Mheshimiwa Waziri wa Mipango wakati huo, aliyekuwa anaitwa Mhe. Tom Mboya. Sera ile, ilisema kuwa tumepata uhuru na tunakusanya ushuru. Je, tutatumia mbinu gani ili tuendeleze Kenya kwa haraka zaidi? Katika Sera ile ambayo ninaangazia ya Sessional Paper No.10 of 1965, ilisema ya kwamba tupeleke pesa nyingi zaidi katika maeneo ambayo yana rutuba na maeneo ambayo yana mvua nyingi. Ule wakati, Sera ile ilikuwa ni sawa kwa sababu, tungepeleka pesa katika Maeneo ya Kati ama Central Kenya, watu wapande kahawa, wapande majani chai ili tuuze ngámbo, tupate ushuru, tuajiri wananchi na tupate fedha za kigeni. Tulistahili kupeleka pesa Mkoa wa Magharibi ama Western Kenya; watu wapande miwa, tutengeneze viwanda vya sukari, watu waajiriwe, tupate ushuru na pia tupate ajira kwa wananchi wetu. Pesa zingine nazo ziende Bonde la Ufa ama North Rift. Watu pia wapande kahawa, majani chai na kadhalika. Bi. Spika wa Muda, lakini miaka 50 baada ya hiyo sera kupita, hatukuweza kuwa na mipango yoyote ya kuhakikisha kwamba maeneo ambayo yanaachwa nyuma kimaendeleo, yataendelea namna gani. Ule usawa ulikuja wakati wa hii Katiba ya mwaka wa 2010. Juzi tumepitisha sheria ya kugawanya pesa kati ya Serikali ya Kitaifa na serikali za ugatuzi, almaharufu Division of Revenue Bill (DORB ). Tulishangazwa na Maseneta ambao walikataza magatuzi yasipate pesa zaidi. Ni jukumu la Maseneta wote ama Seneti kulinda ugatuzi. Hii sheria ya"
}