GET /api/v0.1/hansard/entries/1236746/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1236746,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236746/?format=api",
    "text_counter": 415,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Bi. Spika wa Muda, asante. Tumekuwa na rafiki yangu, Sen. Cherarkey, kwa hili Bunge na tumefanya mambo mengi pamoja. Bi. Spika wa Muda, nafikiri kulikuwa na Ripoti ya Kamati ya Fedha na Bajeti ambayo ilikubaliana na Commission on Revenue Allocation (CRA), ya kwamba magatuzi yanafaa kupata Kshs407 bilioni. Kamati hiyo ya Fedha na Bajeti inayongozwa na mstahiki gavana party leader Sen. Ali Roba, ilileta mabadiliko katika Mswada uliotoka katika Bunge la Kitaifa. Ilikuwa inasema ya kwamba tupatie magatuzi Kshs385 bilioni. Kamati yetu ikasema tufanye mabadiliko na tupee magatuzi Kshs 407 billioni, kulingana na mapendekezo ya CRA. Bi. Spika wa Muda, ukweli ni kwamba - and facts are stubborn - Maseneta 22 walisema ya kwamba Serikali ya Kitaifa haina pesa na kwa hivyo, tupee magatuzi Kshs385 bilioni. Kama si hivyo, basi, tuangalie HANSARD ya hii Seneti. Bi. Spika wa Muda, kwa kuendelea, ---"
}