GET /api/v0.1/hansard/entries/1236781/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1236781,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236781/?format=api",
"text_counter": 450,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda. Kama hizi pesa zilikuwa za kujenga barabara, ukweli wa mambo ni kwamba hatuna mabarabara Taita-Taveta. Ile barabara ambayo iko Taita-Taveta ni ya kitaifa ambayo inatoka Nairobi kwenda Mombasa na imepitia Taita-Taveta, kutoka Mtito wa Andei kwenda Mackinnon Road. Ile barabara ambayo iko Taita-Taveta ni barabara ya kitaifa ambayo imetoka Voi kwenda Taveta na kwenda Holili, Tanzania. Barabara ambayo iko katika kaunti yetu ambayo iko na lami ni barabara kutoka Mwatate kwenda Wundanyi na hizo ni kilomita 15. Katika eneo bunge la Wundanyi pekee yake, tuko na kilomita mbili pekee yake. Hiyo ndiyo eneo bunge, Kenya nzima, ambayo iko na barabara kidogo zaidi ya kilomita tatu. Kama ule mgao wa kusawazisha pesa za kaunti ulikuwa wa kutengeneza barabara, tuko na barabara nyingi katika Kaunti ya Taita-Taveta ambazo hazijatengenezwa, zikiwemo barabara za kutoka Maungu kwenda Kasigau na kutoka Voi kwenda Mbololo hadi Ndii. Kutoka Weruga kwenda hadi Mgambonyi. Kwa hivyo, barabara bado hatujapata na tulihitaji hizo pesa za kusawazisha maendeleo ya maeneo. Bi. Spika wa Muda, kama ni mambo ya maji, hatuna maji na tunaendelea kutengwa. Serikali ingepatia Kaunti ya Taita-Taveta pesa kidogo kupitia kwa hii pesa ya usawazisaji ama Equalization Fund ama kutoka pesa yeyote tufanye miradi ya maji. Tungetoa maji kutoka Lake Chala Taveta, tukaletea watu wa Taveta Mwatate wakafanye ukulima. Tungetoa maji kutoka Mzima Springs tukapelekea watu wa Taita- Taveta. Leo hii maji ya Mzima Springs Phase 1 yanatoka Taita-Taveta lakini watu wa Taita-Taveta wanapata maji kidogo sana. Maji mengi yanaenda Kaunti za Kilifi, Kwale na Mombasa. Mkaazi wa Taita-Taveta hana maji. Tungepata pesa hii ya Equalization, tungetoboa bomba la maji la Mzima Springs"
}