GET /api/v0.1/hansard/entries/123769/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 123769,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/123769/?format=api",
    "text_counter": 349,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Asante sana Bw. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Hoja hii inayohusu wakongwe na wazee wa nchi hii. Nataka kumshukuru Waziri na Wizara yake kwa mambo muhimu sana walioweza kuyajadili na kuyaleta mbele ya Bunge hili ili yaweze kuungwa mkono, huku tukizingatia na kufahamu kwamba wazee wameteseka sana katika nchi yetu. Nchi zingine duniani haswa zile ambazo zimeendelea, zimeweka mikakati ya kuwasaidia wakongwe. Wahenga walisema kwamba palipo wazee hapaharibiki jambo. Kwa hivyo, tunastahili kuwalinda wazee wetu kwa kuwafanyia mambo yanayofaa. Bw. Naibu Spika wa Muda, ninataka kumuuliza Waziri kwa unyenyekevu, aangalie zaidi pesa anazotoa; Kshs1,500. Ikiwa Serikali italipa watu milioni moja na nusu, pesa hizo zitakuwa nyingi sana kwa kila mwezi. Pesa zinatatiza sana na zina tamaa! Mpango ambao anatarajia kutumia kugawa pesa hizo unaweza kuleta madhara makubwa sana, na wale ambao wanatakiwa kufaidika kutoka kwa pesa hizo wanaweza kukosa. Hii ni kwa sababu tumeona kwamba, kupeana pesa tu kupitia Wakuu wa wilaya na tarafa, ni jambo limekuwa ngumu sana. Bw. Naibu Spika wa Muda, unakubaliana nami na Bunge hili kwamba, hata kutoa chakula cha msaada imekuwa ni shida. Chakula kinatolewa, lakini hakiwafikii watu kule mashinani. Kinapotelea hapa katikati. Chakula hiki hakipotei kupitia kwa raia bali kwa wakuu wa Serikali. Kwa hivyo, ningemhimiza Waziri ajenge makao ya wazee. Pesa hizo ni nyingi mno; na ukichukua Kshs1,000 katika kila mwezi kutoka kwa pesa ambazo zinatolewa kila mwaka, zinatosha kujenga makao katika kila mkoa; iwe ni makao mbili au ni moja ambao inamudu watu kati ya 300 na 500. Makao hayo yatasaidia sana kwa sababu Serikali itaweza kuwapatia wazee chakula wakiwa pamoja; na pesa zile hazitapitia katika mifuko ya watu na kupotea. Bw. Naibu Spika wa Muda, vile vile, katika makao hayo, kunawezwa kujengwa hospitali. Hospitali hazitakuwa za kusaidia wale wazee tu, bali zitawahudumia"
}