GET /api/v0.1/hansard/entries/123771/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 123771,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/123771/?format=api",
"text_counter": 351,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "wanaokuja, wachanga na watu wa umri wa kati, ili tuweze kuleta tabasamu ya kupendeza katika utumishi wa Taifa. Bw. Naibu Spika wa Muda, ukiangalia mambo yale tunapatia kipaumbele, wakati mwingine, hatuyachunguzi sana. Tukubaliane kwamba Kshs1,500 kwa kila mtu ni pesa nyingi sana. Pesa hizi zikiwekwa pamoja zinaweza kufanya kazi kubwa sana. Lakini zikiwa zinagawa na kupeanwa, zitaweza kupotea hata kwenye upepo. Kwa hivyo, ninataka Waziri afikirie sana, hata kama amechelewa kufanya hivyo mwaka huu; mwaka ujao, anaweza kujenga makao ya wazee na wasiojiweza ili waache kutaabika. Watu hawa wanasumbuka sana. Katika nchi yetu na Bara la Afrika, sisi hatuzingatii mambo ya wazee; wanadhulumiwa na kunyanganywa mali yao, wengine wanawauliza watakufa lini ili wachukue mali yao. Kwa hivyo, ninataka Waziri achunguze sana mambo hayo. Kwa hayo machache, napenda kuchangia"
}