GET /api/v0.1/hansard/entries/1238041/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1238041,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1238041/?format=api",
"text_counter": 91,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Sen. Kibwana aliniomba nimwakilishe kwa sababu hatakuwa katika Kikao hiki. Nataka kutoa taarifa kuwa Sen. Kibwana hataweza kuendelea na kauli yake. Bw. Spika pia nataka kuomba ruhusa kwa heshima na taadhima katika upeo wa kuketi wa Bunge la Seneti, kunao waheshimiwa wa Bunge la Kaunti ya Kilifi pamoja na baadhi ya wafanyikazi wa Kaunti ile. Kwa sababu nilikuwa nimechelewa naomba unipe dakika moja nijiunge nawe pamoja na maseneta wenzangu kuwakaribisha. Nawashukuru kwa kuja katika Bunge la Seneti ili wajifunze mengi wasiofahamu."
}