GET /api/v0.1/hansard/entries/1238201/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1238201,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1238201/?format=api",
"text_counter": 251,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii ili nitoe mchango wangu kuhusu ripoti ya Kamati ya Ugatuzi na Mahusiano kati ya Serikali za Kaunti na Serikali Kuu. Ninampongeza Sen. Mo Fire maarufu Mwenda Gataya, kwa kuwasilisha suala hili mbele ya Kamati ya Bunge la Seneti. Ni masikitiko kuwa Kaunti ya Tharaka Nithi imekaa zaidi ya miaka 10 bila pahali mwafaka ambapo Bunge la Kaunti linaweza kuketi na kujadili masala yake. Ni masikitiko makubwa. Haya yamechangiwa pakubwa na utepetevu katika tume ya kupambana na ufisadi nchini. Badala ya kuchunguza ufisadi ili wahusika wapelekwe mahakamani, wao wenyewe wanajihusisha katika visa vya ufisadi. Kazi imekwama na hakuna njia yoyote imetolewa kushugulikia suala hili hadi sasa. Yaliyoko Kaunti ya Tharaka Nithi ni sawa na yale yaliyokuwa katika Kaunti ya Kwale, wakati walipokuwa wanajenga Bunge la Kaunti. Mwaka wa 2019, tulizuru Kaunti ya Kwale na ikawa pia ujenzi wa makao makuu ya Bunge la Kaunti ya Kwale ulikuwa umegubikwa katika ufisadi. Kwa hakika, makatibu watatu walipoteza kazi kwa sababu ya hilo suala hilo la ufisadi. Bw. Naibu Spika, ijapokuwa Kaunti ya Kwale ina County Assembly, mpaka sasa hatujaona aliyeshtakiwa kutokana na ubadilifu wa pesa za kaunti ile. Haya ni masikitiko makubwa. Ijapokuwa tunakubali ripoti hii kwa kiwango fulani bado ina mambo mengi ambayo yanatatiza. Kwa mfano, kwenye ripoti, pesa zilizotumika mpaka sasa ni zaidi ya Kshs 217 millioni ambazo zilikuwa zimekadiriwa kutumika kujenga ujenzi huo. Nimeona kuna pendekezo kwamba wakubaliane na pendekezo lililotolewa na mhe. Rais kwamba gharama ipunguzwe mpaka Kshs200 millioni. Ikiwa tayari zaidi ya Kshs200 millioni zimetumika, itakuwaje gharama ipunguzwe irudi chini? Baada ya Kamati kutoa suluhisho, imependekeza kamati nyingine ichaguliwe. Baada ya kutoa suluhisho kwa matatizo yaliyoko, tunatoa nafasi ya kubuniwa kwa kamati zingine ambazo zitazidi kuchelewesha kutatuliwa kwa jambo kama hili. Mimi sikubaliani na wazo la Kamati kwamba kuchaguliwe kamati nyingine ambayo wanaita multiagencyagencies kwa Kiingereza ili iweze kuchuguza suala hili. Bunge la Seneti linashughulikia masuala ya ugatuzi. Hili ni suala la ugatuzi. Kwa hivyo, inafaa swala hili liamuliwe kwa ufasaha na ukamilifu."
}