GET /api/v0.1/hansard/entries/1238203/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1238203,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1238203/?format=api",
    "text_counter": 253,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Sen. Cherarkey, katika mazungumzo yake, amesema kwamba Serikali imetoa Kshs385 billioni katika mwaka wa 2023/2024 kwa mgao wa fedha. Tukiangalia makadilio ambayo Serikali ilipeleka Bungeni ya mwaka wa 2023/2024, wanatarajia kukusanya zaidi ya Kshs2.571 trillioni ambazo ni ongezeko la asilimia 17. Haiwezekani kwamba Serikali itapata ongezeko la asilimia 17 katika mapato yake, halafu itoe chini ya asilimia tano ya zile pesa ambazo itakusanya katika mwaka wa 2023/2024 wa kifedha. Sen. Cherarkey anatupotosha mawazo kwa kusema kwamba tayari Serikali imetoa pesa nyingi tukilinganisha na pesa ambazo zitakusanywa na Serikali katika muhula huu. Pesa hizi zote zinakusanywa katika kaunti zetu. Hakuna mahali ambapo Serikali inasema kwamba hakuna kaunti. Kenya nzima imegawanywa katika kaunti 47. Kwa hivyo, pesa zile zinakusanywa katika kaunti zetu. Hazikusanywi mahali ambapo ni pa Serikali kuu pekee. Bunge la Kaunti ya Tharaka Nithi, linahitaji mahali ambapo wanaweza kukaa na kufanya mijadala yao kama Bunge lolote lile. Wakati Bunge la Tharaka Nithi linakaa, linaheshima kama Bunge la Seneti ama Bunge lolote katika ulimwengu. Ni lazima wapate mahali ambapo watakaa na kufanya mijadala yao bila kuingiliwa kwa njia yoyote. Bw. Naibu Spika, ninaunga mkono ripoti lakini ikarabatiwe tena. . Kwa sababu, masuala mengi ambayo yamezungumziwa katika ripoti hii, ni ya kuregesha nyuma. Tutakuwa tunarejea nyuma kufanya mjadala wakati mambo ni wazi. Pesa ziachiliwe kwa sababu hakuna sheria inayosema kwamba tume ya EACC inaweza kuzuia pesa zisitumike katika muhula ambao zimepangiwa. Zaidi ya miaka kumi imepita bila ujenzi kutendeka. Huo ni utepetevu wa hali ya juu kwa tume ya EACC kutoa pendekezo ama kuzuia pesa zisitolewe wakati hawana maelezo yoyote kuhusu wapi wamefikisha uchunguzi wa ubadilifu wa pesa ambao ulikuwa umepangwa kutokea. Mwisho, naipongeza Kamati. Lakini ni lazima wajitahidi wafanye kazi zaidi ili kuhakikisha kwamba ripoti hii ina manufaa kwa Kaunti ya Tharaka Nithi, Bunge la Kaunti na Sen. Gataya Mo Fire. Asante, Bw. Naibu Spika."
}