GET /api/v0.1/hansard/entries/1238217/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1238217,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1238217/?format=api",
    "text_counter": 267,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Bw. Naibu wa Spika, ningependa kunukuu kutoka kwa Sheria na Kanuni za Bunge 110 kwamba Seneta anaweza kuhairisha jambo lolote hadi wakati mwingine. Haya ni kwa mapendekezo ya Mwenyekiti ili yale ambayo yanajadiliwa kwa sasa, yaweze kupewa muda zaidi ili mapendekezo ambayo Maseneta wameweza kutoa kwa siku ya leo yaweze kuorodheshwa ama yawekwe kama mchango katika ripoti ya Kamati ya Ugatuzi. Hii ni kwa sababu, hatuwezi tena kuanza kusukuma gurudumu upya ilhali tuko na nafasi kama Seneti kukata kauli mara moja na kuamrisha fedha hizi ziweze kutumika mara moja katika ujenzi wa makao makuu ya Kaunti husika. Kwa hayo, naomba kwamba tuairishe kikao hiki ili tuwape Maseneta muda kuchangia na kutia kikomo mjadala huu katika jumba la Seneti. Naomba ndugu yangu jirani aweze kung’atuka kwenye kiti na aniunge mkono. Asante, Bw. Naibu Spika."
}