GET /api/v0.1/hansard/entries/1238295/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1238295,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1238295/?format=api",
"text_counter": 345,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Tulipoenda Shakahola juzi, tulipata kwamba zaidi ya watu 110 walipoteza maisha yao kwa sababu ya mafunzo ya itikadi kali ya mmoja wa wanaojiita makasisi au mapasta katika eneo lile. Pasta yule amekwenda kortini na kutoka kama mara 50. Kuanzia mwaka wa 2018, Serikali ilikuwa inajua kwamba alikua akifundisha watoto wasiende shule na ana itikadi ya kufundisha watu wasiende hospitali wakiwa wagonjwa. Lakini Serikali ilimuangalia tu."
}