GET /api/v0.1/hansard/entries/1238466/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1238466,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1238466/?format=api",
    "text_counter": 133,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Miraj",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Ingekuwa vyema kama Waziri angefahamisha Bunge hili kiwango cha fedha ambazo Kenya imepoteza. Hivi sasa kila mahali wenzetu wanazungumza kuwa uchumi na dola imepanda juu zaidi ya shilingi. Haya yote ni kwa sababu ya vile vitendo vya ukosefu wa nidhamu vinavyoendelea kutoka kwa upande ule mwingine wa Bunge hili. Tumeona Maseneta wakizunguka jana na hayo ndiyo maswala uliyoyazungumzia. Tafadhali ningependa unukuu zile pesa ambazo uchumi wa Kenya umekosa kwa sababu ya maandamano katika taifa letu."
}