GET /api/v0.1/hansard/entries/1238908/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1238908,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1238908/?format=api",
    "text_counter": 212,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "wakaribishwe kule wakague. Lakini pia matatizo yale pia yasionekane ni ya sasa hivi. Uzuri utajulikana ni akina nani ndio waliofanya makosa katika miaka iliyopita. Hao wakija kule watasaidia maanake kuna matatizo ambapo saa zingine bursary inatumika kisiasa, saa zingine bursary haiendi kwa watarajiwa, na saa zingine kuna shule ambazo kuna wakora ambapo inakubidi ukague pesa ya bursary moja kwa moja mpaka ukosane na walimu. Kama hufanyi hivyo, imekuwa ni kama biashara. Ninataka huyo Auditor-General kwa hii Ripoti yake pia ahakikishe amekagua vizuri hizi shule. Shule pia zina matatizo mengi. Kwa hii NG-CDF, tulipoingia, wale walio na wadi tatu wamepunguziwa. Ni masikito kwa sababu sijui walitumia mbinu gani kupunguza na imekuwa kila mtu anazungumza mambo ya one man, one shilling, one vote . Watu wengine wanatutolea bahati eti kwa nini watoto wetu wanaenda kusoma shule zao. Ukienda zile shule pengine zimetengenezwa hizi boundary walls au hizi kuta zilijengwa kutoka wakati wa ukoloni. Sisi zetu hazina mpaka itabidi tutegemee mfuko huu kuzitengeneza ambapo hata sasa hatuwezi kupanda miti. Wanaambiwa kwa NG- CDF wapande miti lakini hauwezi kuipanda hadi utengeneze kuta. Na ukitengeza kuta inaweza chukua miaka kumi ndio imalizike na hizo ni kuta peke yake. Utakosa kufanya jambo jingine kwa sababu pesa imepunguzwa. Ingekuwa vizuri Kamati ya Bunge itembelee maeneo yaliyona wadi tatu ili iangalie matatizo walionayo, iboreshe zile shule, itafute mbinu kabla ya kufikiria mambo ya one man, one shilling, one vote . Mwanzo mumeinua wengine maanake matatizo ni mengi kwa shule. Tukiendelea hivi, itabidi hawa watoto wetu waje huko kwenu vivyo hivyo. Ni lazima mtafute mbinu za kutusaidia hata kama ni kwa mfuko mwingine; angalau ukuta wa mpaka ujengwe ili sisi tufanye mengine. Hii ni kwa sababu mambo mengi hayajafanyika kwa muda mrefu na yameleta shida na kuendeleza mgogoro. Bw. Spika wa Muda, mambo haya yanasikitisha. Shule zimetajwa nyingi kama vile Kiwayu, Mkunumbi, Matondoni na Witu. Pesa nyingi zimetajwa pia na inasikitisha kuwa huwezi kuona pesa iliyotumika pale. Nimesikia Wabunge wakizungumza na ni kwa utovu wa ufahamu na hawaelewi mambo kwa kuwa hawajazunguka Kenya hii na kuona jinsi mazingira yalivyo. Kuna mmoja aliyesema kuwa Pwani ina matatizo na gharama za kujenga ziko juu, lakini kama angekuwa na ufahamu, basi hasingesimama na kusema vile kwa sababu Lamu Mashariki ina changamoto tofauti. Kwa mfano, mafuta ya meli itakayotumika kutoka Lamu kuenda mahali pa dakika ishirini itatosha kuja Nairobi na kurudi. Sasa lazima gharama za usafiri ziwe nyingi na ukisema Pwani, ni lazima useme ni wapi? Huwezi kufananisha mtu wa Nairobi kwa kusema kuwa gharama yake ya kujenga darasa itakuwa sawa na mtu wa Kiunga. Kandarasi inapotolewa kule, hata mtu anakataa kufanya. Kwa mfano, sasa hivi tunataka kutengeneza barabara na pesa zimetolewa lakini ni mpaka meli itoke Mombasa ibebe vifaa hivyo kupeleka Mtagawanda, ambapo ni dakika ishirini tu kutoka Lamu. Lakini meli hiyo inatoza pesa ngapi? Inaweza kulipisha zaidi ya Ksh6 milioni kusafirisha vifaa pekee yake. Kwa hivyo, mkizungumzia gharama za usafiri, ni lazima mtaje mahali husika. Kamati inafaa kutembelea sehemu hizi. Hakuna Al Shabaab na mnafaa kuona changamoto. Kwa hivi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}