GET /api/v0.1/hansard/entries/1239169/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1239169,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1239169/?format=api",
"text_counter": 148,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Bw. Spika, asante kwa nafasi hii. Ninadhani alicholeta Sen. Cherarkey ndani ya Bunge hili, ni kwamba kuna matapeli katika Serikali. Vile vile, kuna nyenzo ama lemba zao katika shirika la ndege ambao wako na mkataba wa kupora na kupunja pesa za umma. Haiwezekani mtu kurejesha matokeo ya kuanguka mtihani ama kipato cha shirika hilo kwenda chini, na Serikali inampigia makofi na kutia sahihi kandarasi mpya. Ni kinaya sana."
}