GET /api/v0.1/hansard/entries/1239171/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1239171,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1239171/?format=api",
"text_counter": 150,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Sijaona Waziri au mtu yeyote katika Serikali, akikashifu Shirika hili kwa matokeo duni jinsi tunavyoona. Juzi tumeona wenzetu Mombasa wakilalamika kwa sababu shirika hili lilifutilia mbali shughuli zao kule Mombasa na kwenda mpaka nchi za ughaibuni. Kwa sababu wameshindwa, sasa wengine hawapaswi kufua dafu katika usafiri wa ndege. Mimi ninaunga Sen. Cherarkey mkono. Iwapo wameshindwa, wafunge shirika hilo kabisa. Milango ifungwe, watu wafukuzwe waende nyumbani na tuanze upya kwa karatasi jipya lisilo na dosari yoyote. Iweje mabilioni yamezwe na walafi kupitia shirika hili, ilhali kuna viwanda vya sukari na kuna wakulima wachochole mashinani ambao hawana pesa? Tutamlilia nani iwapo Serikali haisikii? Mimi ninaomba tusimame na Wakenya ambao hawajawahi hata kupanda ndege wala hawajui ndege inavyofanana. Tusije hapa na tukawapigia makofi wanaojivinjari kwa ndege, ilhali walio chini wanaomba Mungu: “Ee Mungu rabuka, tulikukosea nini?’ Asante, Bw. Spika."
}