GET /api/v0.1/hansard/entries/1239206/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1239206,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1239206/?format=api",
"text_counter": 185,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chute",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13583,
"legal_name": "Chute Mohamed Said",
"slug": "chute-mohamed-said"
},
"content": "Bw. Spika, sijui hiyo “State capture” ni gani. Tusilete tu hapa Statements pekee yake. Wiki mbili zilizopita, Waziri wa Barabara alisema Kenya Airways ni private company. Kwa hivyo, hawataulizwa maswali katika Bunge. Kama hatuwezi kuwauliza maswali, basi wacha tumuambie Mhe. Raila aende afanye maandamano asimamishe hao watu kazi. Kama sisi tumeshindwa kusimamisha hawa watu kazi, basi tutumie yule mtu ambaye ataweza kuwasimamisha. Kisheria, sisi hatuwezi kuwasimamisha kwa sababu contract imesainiwa ya miaka 25. Kama hatutoki, basi twende tuvunje hizo contract zao. Bw. Spika, nikiunga Sen. Cherarkey mkono, ningependa tusiongee mambo ya kusema ati tunafanya hii na hakuna kitu kinachofanyika. Statement pekee yake haitatusaidia. Kama inawezekana, inquiry ifanywe na tuhakikishe hiyo kitu imesimama. Jambo la mwisho, kuna mjadala unaendelea ambao unasema hii airline tuiuze ama tuiongezee pesa. Ukitoboa debe hapo chini, hata ukiweka maji namna gani haitajaa. Hiyo kampuni iuzwe, inunuliwe na kampuni kama Emirates ama Ethiopian Airlines ili Kenya ipate hizo pesa tuingize kwa mashamba yetu. Asante sana, Bw. Spika."
}