GET /api/v0.1/hansard/entries/1239593/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1239593,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1239593/?format=api",
    "text_counter": 197,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa nafasi hii. Ningependa kuchangia Taarifa ya Sen. Okenyuri kwamba walimu wa nchi wanachekwa na jamii. Ukiangalia jinsi taasisi inayohusika na maswala ya walimu huharakisha na walimu hawapati nafasi kufanya kazi zao za ziada ili kuongeza kipato. Ukiangalia jinsi walimu hawa wamekuwa wakisahihisha mitihani hii na mchakato mzima, inastahili Serikali iwe imetenga fedha za kuwalipa walimu hawa baada ya kazi zao. Baadhi ya walimu hawa wana mikopo kwenye benki na mashirika mengine. Ni jambo la busara Serikali kuwalipa walimu kwa kazi waliyoifanya. Kando na kulipa kwa kusahihisha, ni walimu hao ndio hufunza wanafunzi ambao hubobea na kupata matokeo ambayo huwafurahisha wengi. Mimi kama mwalimu, najiunga na Seneta mwenzangu hapa, kurai Wizara ya Elimu na taasisi husika ya mitihani kwamba iwapo wataandaa mitihani, lazima watenge pesa ziwe tayari kuwalipa walimu pindi wanapomaliza shughuli ya kusahihisha mitihani. Jambo hili linaendelea kudhihirika katika idara ama tume ya kusimamia mipaka na kura. Wale ambao walisimamia kura za useneta wa Bungoma na maeneo mengi hapa nchini, vile vile wanaendelea kupiga miayo na kupanguza machozi ilhali sisi kama viongozi na Serikali hatutilii manani kilio chao kama Wakenya ambao wanastahili kulipwa kwa jasho lao. Naomba Serikali na taasisi husika kulipa walimu na waliohusika katika uchaguzi ili mfumo wa chini-juu uweze kudhihirika Kenya nzima jinsi tunavyotekeleza majukumu yetu. Asante sana, mhe. Spika."
}