GET /api/v0.1/hansard/entries/1240367/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1240367,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1240367/?format=api",
"text_counter": 590,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Asante sana Mhe. Spika wa Muda. Swali langu laenda kwa Waziri hivi: Tumepata kuwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mombasa, Kampuni ya Umeme ilizima stima hosipitali na ikaleta maafa hasa kwa watoto waliokuwa ndani ya incubators na wagonjwa waliokuwa ndani ya chumba cha watu mahututi. Huo ni wakati ambapo walikuwa wanaelewa kuwa Serikali haikuwa imetoa mgawo wa kifedha wa majimbo na walikuwa bado wanahangaika. Ni mbinu gani ambayo unaweka, kama Waziri, kuonyesha kuwa waweza ukasimama pamoja na wagonjwa hospitalini katika kusambaza stima na kuhakikisha kuwa ikiwa kuna deni, basi liweze kupelekwa kwa utaratibu lisiweze kuleta maafa?"
}