GET /api/v0.1/hansard/entries/1240994/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1240994,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1240994/?format=api",
    "text_counter": 68,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Hii Petition imekuja wakati mzuri sana, kwa sababu, kule Kwale Kaunti yangu nina kesi nyingi za walimu kama hawa ambao hawajalipwa pesa zao. Ni jambo la kusikitisha sana haswa kwa walimu. Walimu wamesomesha wanafunzi na wanafunzi wakafaulu. Lakini utakuta kwamba walimu mpaka leo wanalia wakitaka kulipwa pesa zao. Sijui shida iko wapi? Nina kesi karibu tano za walimu. Walimu wawili wameshafariki. Kuna mwingine juzi alipata ajali. Shida iko wapi katika Serikali. Kwa nini hii Tume ya Teachers Service Commission (TSC) hailipi?"
}