GET /api/v0.1/hansard/entries/1241025/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1241025,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1241025/?format=api",
    "text_counter": 99,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii. Kuanzia mwanzo, ninaunga mkono dua hili ambalo limeletwa na Sen. Thnag’wa kwa sababu ya shamba la familia ya Mbogo Wainaina kuchukuliwa. Mambo ya mashamba katika Jamhuri yetu ya Kenya imekuwa ni donda sugu. Watu wengi wamekuwa wakigandamizwa na wale ambao wanafikiria wako na nguvu kuliko wegine. Kwa hivyo, ninakubaliana na Sen. Thang’wa ya kwamba, familia ya Mbogo Wainaina imefanya vizuri kuleta taarifa hii. Wamefanya jambo lingine muhimu kwa kusema kwamba wanapatia jukumu Kamati ya Ardhi, Mazingira na Maliasili ambayo iko katika Senenti hii. Wanauhakika na wanaamini ya kwamba itaweza kutenda haki. Ndiposa kulingana na taarifa yenyewe, wanasema ya kwamba itafute ni nani mwenye shamba lile kamili. Hawasemi ni lao wala ni nani. Hii ni kwa sababu ni watu ambao wanapenda ukweli na wana imani na Kamati ya Seneti ya kwamba itafanya haki."
}