GET /api/v0.1/hansard/entries/1241027/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1241027,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1241027/?format=api",
    "text_counter": 101,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Bw. Spika, ningependa hii familia ya Mbogo Wainaina itendewe haki na waweze kupewa fidia kwa kugandamizwa. Ni vizuri wakati Kamati hiyo inashughulikia jambo hili, iangalie maswala mengine katika sehemu hiyo ya Kaunti ya Kiambu. Ukitembea sehemu nyingi za nchi yetu ya Kenya, kuna shida za mashamba ambazo zinafanya watu wauane. Kwa hivyo, ningependa kuuliza Kamati hiyo, wakati wanashughulikia swala hili, washughulikie hata sehemu zingine. Ukitembea Kaunti ya Laikipia, upande wa Marmanet, watu walifurushwa kutoka mashamba yao na wanapaswa kilipwa fidia. Ukitembea sehemu za Matanya, vile vile, kuna ile shida. Unapata watu wametolewa katika mashamba yao na wanaishi katika maisha ya uchochole. Kwa hivyo, kwa sababu Wakenya wanaimani na Seneti, hasa Kamati hii ambayo inaongozwa na Sen. Methu, ninahakika watafuatilia lile jambo kwa kindani ndio hawa ndugu zetu waache kuwa na hii shida na waweze kupewa fidia na kuishi maisha wanayopaswa kuishi. Bw. Spika, ukitembea sehemu zingine hapa Kenya, tuko na mashamba yetu lakini hatuwezi tukaishi kwa sababu ya kutokuwa na usalama. Kwa hivyo, jambo la mashamba limekuwa donda sugu. Ukitembea mahali panaitwa Kimanju, Ilipolei na Dol Dol, hiyo ndiyo shida; watu wanapigwa na wanaondolewa. Jambo kubwa, watu wanapofanya hivyo, wanataka kujinyakulia mashamba. Kama vile Sen. Cherarkey alivyosema, wewe ukiwa Mwafrika, huwezi ukaitwa mwanamme kama huna shamba. Unapata wengine wanatumia nguvu walizonazo kuwagandamiza wengine. Kwa hivyo, Kamati ambayo itashughulikia jambo hili la Ardhi, Mazingira na Maliasili iangalie kwa kindani na walete suluhu la kudumu. Nashukuru kwa kunipa muda huu."
}