GET /api/v0.1/hansard/entries/1241057/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1241057,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1241057/?format=api",
    "text_counter": 131,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Mhe. Spika. Nimesimama kuunga mkono maombi ya taarifa ya Sen. Chimera kuhusiana na Taarifa ya kwanza. Hili swala la wakaazi wa Ukunda ambao ardhi yao ilichukuliwa kwa sababu ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa Ukunda ni swala ambalo limekuwa donda sugu. Ninakumbuka, tulizuru mahali pale mnamo mwaka 2018 tukiwa na Kamati ya Fedha, ikiongonzwa na Sen. M. Kajwang’. Wahusika pia walikuja katika Bunge hili la Senate kueleza masaibu yanayowapata kwa ucheleweshaji wa kulipwa kwa ile ardhi ambayo ilichuliwa. Kwa hivyo, ni jambo ambalo limekuwa donda sugu. Niliona juzi Kiongozi wa Serikali alisema ya kwamba National Land Commission (NLC ) wasijihusishe na mambo ya kutathmini ardhi ambazo zinachukuliwa kwa miradi ya Serikali."
}