GET /api/v0.1/hansard/entries/1241059/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1241059,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1241059/?format=api",
    "text_counter": 133,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Swala hilo ni kwamba tunapita mipaka ya sheria kwa sababu sheria inasema ya kwamba, maswala ya kutathmini, yaani valuation, ni swala ambalo litafanywa na NLC. Ikiwa Rais wa nchi atasema ya kwamba ameikataza NLC wakati sheria inairuhusu NLC ifanye kazi hiyo, ina maana ya kwamba anaingilia kazi za tume huru katika nchi yetu ya Kenya. Tunaomba NLC iharakishe ulipaji wa watu hawa na sehemu yoyote nyinyine ambayo ardhi imechukuliwa na watu hawajalipwa, walipwe kwa haraka. Hata hivyo, tunapinga vikali kauli ya Rais kusema ya kwamba NLC hawataweza tena kutathmini ardhi ambazo zinachukuliwa kwa miradi ya Serikali. Asante, Bw. Spika."
}