GET /api/v0.1/hansard/entries/1241185/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1241185,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1241185/?format=api",
    "text_counter": 259,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Beth Syengo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kwa mfano, katika Kaunti yangu, ninajua ndoa iliyovunjika kwa sababu mama aliamua kufanya biashara ili aboreshe maisha yao. Mama huyo aliomba pesa kwenye kikundi cha kukopesha na kuanza biashara. Mwaka ulipopita bila kulipwa, mwanaume alimwambia kuwa aliomba pesa zile ili wawe maskini. Maana mali ya familia itawekwa kwenye mnada. Mabati ya nyumba ilitolewa, baiskeli na sufuria zilichukuliwa. Nyumba ile ilikumbwa na shida tupu, hadi mume na mke wakaachana."
}