GET /api/v0.1/hansard/entries/1241186/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1241186,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1241186/?format=api",
    "text_counter": 260,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Beth Syengo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Ikiwa Mswada huu uliopendekezwa na Sen. Mariam Omar utakuwa sheria, itakuwa muhimu kuhakikisha malipo yanafanyika haraka iwezekanavyo ili watu waendelee kukuwa kibiashara. Isikuwe wachache wanapata malipo, ilhali wengine wanahangaika. Malipo ya haraka itasaidia walio chini; wanarika na wamama kupata fedha kwa kujibidiisha kufanya biashara. Watu wanapohangaika, hata vijana wataogopa kujitosa katika ulingo wa kufanya biashara kwa sababu wameona wenzao waliojaribu biashara wakihangaika. Naunga mkono Mswada wa Sen. Mariam Omar. Huu Mswada ni muhimu kwetu kama maseneta. Mswada huu unadhihirisha kwamba tunafikiria mambo muhimu yanayoathiri maisha ya wananchi wa Kenya. Bi. Spika wa Muda, naunga Mswada huu mkono."
}