GET /api/v0.1/hansard/entries/1241249/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1241249,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1241249/?format=api",
    "text_counter": 323,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Shakilla Abdala",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "muda unaotarajiwa. Kama hatapewa malipo yake basi kuna hatua muhimu zitakazochukuliwa. Bi Spika wa Muda, hatua kadha zimependekezwa kuchukuliwa katika Mswada huu ili kuzuia matatizo kama hayo. Kwa mfano, Mheshimiwa mwenzangu ameongea kuhusu kutoza faida ikiwa pesa hizo zitacheweleshwa. Tunaweza kurekebisha pendekezo la kutoza faida katika Mswada huu. Tunaweza kupendekeza kwamba pesa zilipwe vile vile bila faida. Tunapendekeza jambo hilo lifanyiwe amendments. Bi Spika wa Muda, ni lazima mtu akipeana huduma alipwe pesa zake kwa wakati unaofaa. Hakuna haja ya kucheleweshwa. Na wale wahusika pia lazima wawajibike. Kwa mfano, katika kaunti, gavana anapotoka ofisini na mwingine kuingia, lazima kuwe na mipangilio kamili ya kufanya proper handover ya kusema kwamba, “Haya ndiyo mambo ambayo yamebakishwa na hizi ndizo kazi ninazokukabidhi kuendelea nazo katika shughuli zako za miaka mitano.” Wakifanya hivyo, hakutakuwa na hali ambapo gavana ambaye ameingia ofisini aseme kwamba hayo ni mambo ambayo hayamhusu. Saa zingine, utakuta miradi imeachwa katikati baada ya kulipiwa pesa nyingi za mlipa kodi. Yule gavana aliyeingia mamlakani huwa hataki kushugulika kulipa ile pesa na pengine ni kitu ambacho ni cha muhimu au ni huduma ambayo wananchi wanahitaji na wameitisha. Utakuta wale viongozi ambao wameingia mamlakani wanakataa kulipa watu waliofanya kazi na serikali ya kaunti. Kwa hivyo, huu ni Mswada wa maana sana ambao unafaa kupigwa msasa. Mswada huu ukishapigwa msasa kikamilifu kutokana na maoni ya Maseneta, nina hakika huu Mswada utafanya kazi yake nzuri na pia utapunguza zile shida na yale majukumu ambayo yanaachiwa magavana na wenzao ambao wanatoka ofisini. Bi Spika wa Muda, la muhimu ni kwamba huu Mswada unafaa kupigwa msasa halafu upitishwe na Seneti. Asante."
}