GET /api/v0.1/hansard/entries/1241393/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1241393,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1241393/?format=api",
"text_counter": 83,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa kuunga mkono Ardhihali ambayo imeletwa Bungeni na Julius Wairiuku Wanjohi kuhusiana na kutotekelezwa kwa maazimio ya kuwaajiri wafanyikazi katika Kaunti ya Nyeri. Bw. Naibu Spika, ni masikitiko kwamba ni miaka 10 sasa na hao wafanyikazi hawajaandikwa kazi na Kaunti ya Nyeri. Kama tunavyojua, stimulus package ilikwisha, Serikali za kaunti zikaanza kazi na hawa wakasahaulika kabisa kutokana na utepetevu wa Serikali ya Kaunti ya Nyeri. Ningependa kuongezea kuwa hawa wakufunzi wanafanya kazi muhimu. Wale wote ambao hawafaulu kwenda kwa taasisi ama chuo kikuu, hujifunza kazi za mikono katika taasisi hizi ambazo wakufunzi hawa wanafanya kazi. Wanafanya kazi muhimu sana ya kufunza useremala, uashi na nyinginezo. Bw. Naibu Spika, imependekezwa kwamba nyumba ambazo zitajengwa na asilimia tatu ya ushuru, zitahitaji watu kama hawa. Hao ndio wataweka madirisha, milango na kazi za nyaya ambazo haziwezi kufanyika bila wataalamu. Ni muhimu ardhihali hii ifanyiwe kazi kwa haraka kwa sababu tayari wameshangoja miaka 10. Watakaoamua swala hili, wahakikishe kwamba mishahara ya wakufunzi hawa imekuwa back dated. Walipwe kutoka tarehe ambayo mkataba uliwekwa kati ya serikali za kaunti na Transition Authority, iliyokuwepo mamlakani wakati wa mkataba huo. Haitakuwa vizuri wakufunzi hawa kupoteza haki zao ambazo zilikuwa tayari zimekubalika na ni utepetevu tu wa Kaunti ya Nyeri ndiyo umesababisha kikwazo hiki."
}