GET /api/v0.1/hansard/entries/1241397/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1241397,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1241397/?format=api",
    "text_counter": 87,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "ambaye ametoa uongozi na kuapa kwamba atafuata sheria na kanuni za Katiba, kuhakikisha kwamba kila Mkenya ambaye yuko na nafasi ya kazi anawajibika na vilevile anapata kipato kwa jasho lake. vilevile, haya yanadhihirika wakati huu wa Serikali. Kuna wauguzi ambao wanahudumu chini ya mfumo wa Universal Health Care (UHC) na mkataba wao ulikamilika juma lililopita. Mhe. Rais na Serikali yake walikuwa kwa mkutano kule Naivasha. Katika mkutano huo, magavana waliahidi kwamba hawa wachapa kazi, wahudumu wa afya, wataendelea kufanya kazi pasipo bugdha yoyote. Kufikia sasa, wauguzi hawana mbele wala nyuma na hawajui hatima yao iko wapi. Kazi yetu sisi kama Seneti ni kutetea ugatuzi. Wachapa kazi kama hawa wahudumu wa afya na wale ambao wameleta ardhilhali zao kwenye Bunge hili la Seneti, lazima wapewe haki yao, walipwe jinsi inavyotakikana. Tukifanya hivyo, mfumo wa afya na mfumo wa taasisi za vijana humu nchini zitapata nafasi zinazostahili na mgao wao wa bajeti. Bw. Naibu Spika, kwa hayo machache, ninaunga mkono utetezi wa Mkenya huyu. Naomba Kamati husika imwalike Gavana ama vitengo vya kaunti, vijieleze ni kwa nini wanaendelea kunyanyasa Wakenya ambao wamejitolea kufanya kazi, japo kwa kipato kidogo."
}