GET /api/v0.1/hansard/entries/1241399/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1241399,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1241399/?format=api",
    "text_counter": 89,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, asante kwa kunipa hii fursa, nichangie ardhihali ya Bw. Magembe. Ardhihali yenyewe inahusu umuhimu wa kutunga sera, sheria na kanuni za kudhibiti wanaofanya kazi katika soko la ukopeshaji. Ni bayana kwamba pesa zinahitajika na kuna umasikini katika jamii. Lakini, watu wengi ambao wameenda kukopa pesa kwa yale mashirika ya benki ambayo yako nje, wamepata dhiki badala ya faida. Kwa hivyo, kuna umuhimu wa kutunga sera na sheria za kutoa mwongozo kwa wale ambao wanakopesha pesa. Kwa mfano, tuwe na sheria za kuangazia sifa za wale wanaokopesha. Pia, tuwe na sera za kuangazia riba ambazo wakopeshaji watatoa kwa wananchi. Vile wenzangu walivyosema, kuna watu wanaokopesha pesa kwa riba ya juu sana. Wanaitwa shylocks kwa Kimombo. Unapewa pesa kwa riba ya asilimia 30 kwa mwezi. Hiyo riba iko juu sana. Lakini kwa vile uko na shida, labda karo ya mtoto, wengi wamejipata taabani, wakakopa hizo pesa na wakashindwa kulipa. Bw. Naibu Spika, kule kwetu, kuna mtu alikopa pesa lakini kwa vile hakuwa amepata mafunzo mufti, alifanya nyumba yake kuwa hoteli. Alitumia zile pesa vibaya. Asubuhi, anapikia watoto chai, mayai, chapati na mahamri. Ikifika wakati wa chakula cha mchana, anapikia watoto wake pilau, biriani na chapati, wachague. Ilipofika wakati wa kulipia hizo pesa na akashindwa, wakopeshaji walikuja na kung’oa mabati. Ile familia ikawa wako na nyumba lakini haina mabati. Hata mifugo wao walichukuliwa. Bw. Naibu Spika, kwa hivyo, kuna umuhimu. Ninaunga mkono hili ombi la Bw. Magembe, kwamba tuweke sera na sheria za kudhibiti hili soko la kukopesha. Kwa sasa halina udhibiti na tunahitaji kuwatoa watu wetu katika dhiki ili wapate faida. Tunataka Kamati ambayo itaangazia maswala haya, ije na sheria ambayo itadhibiti soko la ukopeshaji la hawa shylocks na wafanyi biashara ndogo ndogo."
}