GET /api/v0.1/hansard/entries/1242341/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1242341,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1242341/?format=api",
    "text_counter": 68,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika. Sio kila siku tunakuwa na Waziri wa Kawi katika Bunge la Seneti. Pia ninaelewa kwamba ninafaa kuuliza swali lingine kutokana na swali asili ambalo Sen. Lomenen aliuliza. Hata hivyo, umuhimu wa sabuni ni povu. Kama Seneta wa Kaunti ya Kirinyaga, kuna masuala ambayo ninafaa kusema. Hata kama sio maswali, mambo hayo yatamwezesha Waziri wa Kawi kwenda na taarifa. Bw. Naibu Spika, ninaomba uniruhusu niseme jambo moja. Nitakuwa sifai kama sitamwambia Waziri kuwa, kuna watu kutoka Kaunti ya Kirinyaga, sehemu ya Gathigiriri, ambao wamekaa miezi mitatu bila stima. Sitakuwa na maana katika Bunge hili, iwapo sitasema Rwama Factory na Muthigiini hawana stima kwa miezi miwili. Sitakuwa na maana kama sitasema watu wa Kagio na Rwang’ondu wanapata huduma za stima kutoka Kenya Power (KP)."
}