GET /api/v0.1/hansard/entries/1242609/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1242609,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1242609/?format=api",
    "text_counter": 91,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu wa Spika. Kabla sijachangia maombi ya Taarifa iliyoletwa Bungeni na Sen. Hamida, ningependa kumkumbusha Sen. (Dr.) Khalwale kuwa hili ni Bunge. Mambo ya Bunge ni mambo ya Bunge na mambo ya Rais ni mambo ya Rais. Kwa hivyo, mambo ya Bunge lazima yazungumzwe Bungeni. Ningependa kuchangia Taarifa kuhusiana na kuachiliwa kwa wafungwa wanaotumikia vifungo vidogo vidogo gerezani. Ninawapongeza Maseneta wa Kenya Women Senators Association (KEWOSA) ambao juzi walizuru gereza la kina mama la Langata, ambapo waliwatoa takriban wafungwa 100. Wafungwa hao walikuwa wamefungwa kwa makosa madogo madogo. Bw. Naibu wa Spika, hii sio mara ya kwanza kwa Bunge la Seneti kufanya ziara ya magereza. Nakumbuka Senate Mashinani ilipokuwa Kaunti ya Kitui, tulizuru gereza la Kitui na kutoa zaidi ya wafungwa 100. Wakati huo, Seneta wa Kaunti ya Nandi ndiye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Sheria na Haki za Binadamu. Seneta mwenyewe sasa amekua mtu wa kukaa back bench ."
}