GET /api/v0.1/hansard/entries/1242611/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1242611,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1242611/?format=api",
"text_counter": 93,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Tulitoa zaidi ya wafungwa 100 kutoka gereza lile. Baada ya hapo, Jaji Mutende aliyekuwa akihudumu katika kituo kile, alifanya ziara katika gereza lile, akaangalia zile faili za wafungwa wote waliokuwa na makossa madogo madogo, na wote wakaruhusiwa kwenda nyumbani. Ni kwa sababu ya kazi ambayo Bunge la Seneti lilikua limefanya. Bw. Naibu wa Spika, ni muhimu swala hili liangaliwe kwa undani. Tulipokuwa tunahudumu katika Kamati ya Haki, Sheria na Haki za Binadamu, tulizuru gereza la Industrial Area. Hapo, wafungwa wanaishi katika hali ngumu sana, hususan wale walioko rumande wanaosubiri kesi zao zimalizwe ndio waende nyumbani. Hao wafungwa wanazuiliwa kwa dhamana ya Ksh5,000 au Ksh10. Mahakama hazijaweza kuzingatia hali ya uchumi na hali ya maisha ya wananchi wa Kenya. Mtu anapelekwa mahakamani kwa makosa madogo, anapewa dhamana ya Ksh20,000 au Ksh100,000 ama atoe title deed au log book . Yote haya yanachangia kujaza wafungwa katika magereza yetu. Kulingana na jinsi hali ilivyo sasa, hairidhishi. Ijapokuwa Serikali---"
}