GET /api/v0.1/hansard/entries/1242628/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1242628,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1242628/?format=api",
"text_counter": 110,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante, Bw. Naibu Spika. Ningependa kuchangia swala hili la madawa katika hospitali zetu. Shirika la KEMSA kwa sasa limepoteza sifa katika Global Fund inayotusaidia kununua na kusambaza madawa. Sijui ni njia gani itatumika kuhimiza Serikali kuchukua hatua ili kurejesha imani na shirika hili. Hivi sasa, shirika hili limepoteza wadhfa wake. Pili, ikiwa hatua zimechukuliwa na watu walio fanya ufisadi wa aina yeyote pale ndani wamejulikana wazi na kufutwa kazi, hilo si jambo la mwisho. Pesa zilipotea na Serikali inafaa kuzifuata. Ninataka kujua nia ya Serikali hii kuhusu jambo hili baada yao kufutwa kazi. Kitendo cha uhalifu hakiwezi kumalizika. Lazima sheria ifuatwe. Waliofutwa wanafaa kupelekwa mahakamani na kushtakiwa ili haki ya wananchi ipatikane. Swala la pili ni kuhusu shule ya watoto viziwi iliyo kule---"
}