GET /api/v0.1/hansard/entries/1242644/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1242644,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1242644/?format=api",
"text_counter": 126,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Tabitha Mutinda",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante Bw. Naibu Spika. Nachukua fursa hii kuwakaribisha wanafunzi wa shule ya upili ya Embakasi. Shule ya wasichana tunayojivunia hapa Nairobi. Nafahamu kuwa wasichana wa shule hii wanatia bidii. Nawahimiza wanafunzi kutia bidii kwenye masomo. Kazi yetu kama Maseneta ni kuangalia shughuli za magavana, vile wanachapa kazi na kutekeleza majukumu yao kama magavana. Pia sisi tulipitia kitengo cha shule ya upili. Pia nyinyi munaweza kuwa hapa tulipo. Wanafunzi, mchukue nafasi hii kupata mwelekeo na mwangaza ambao kesho utawasaidia ili mutimize ndoto zenu. Heshimuni walimu na wazazi wenu wakati wote na mungu awabariki."
}