GET /api/v0.1/hansard/entries/1242699/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1242699,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1242699/?format=api",
"text_counter": 181,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Tabitha Mutinda",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Naibu Spika, nachukua fursa hii kukushukuru kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia Taarifa iliyoletwa na Sen. (Dr.) Murango kuhusu mtoto ambaye vidole vyake vilikatwa katika Hospitali ya Referral ya Kerugoya. Inakuwaje mtoto ambaye anaugua ugonjwa wa pumu kukatwa vidole na madaktari wa hospitali hiyo? Tumeelezwa kwamba madakatari hawajapeana ripoti kwa familia ya mtoto huyo. Ni uchungu sana kwa mzazi. Inasikitisha sana kuona kwamba hospitali za kaunti ambazo Seneti inatetea zinakosa kutimiza majukumu inavyofaa kisheria. Hili ni jambo ambalo Kamati ya Afya inafaa kushughulikia kwa dharura na kuchunguza kwa kina. Tunafaa kupewa ripoti inayoeleza kwa nini mtoto huyo alipoteza vidole vyake akiwa na umri mdogo. Huo ni uzembe wa madaktari wa hospitali hiyo kwa sababu hawajaeleza kinagaubaga kilichosababisha hilo. Bw. Naibu Spika, vile vile, Sen. (Dr.) Murango amezungumzia uchunguzi unaoendelea katika ile hospitali ya kufanya uchunguzi zaidi iliyoko Kerugoya katika Kaunti ya Kirinyaga. Ninge---"
}