GET /api/v0.1/hansard/entries/1242807/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1242807,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1242807/?format=api",
    "text_counter": 289,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murang’o",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Nachukua nafasi hii kwanza, kumshukuru Sen. Beth Syengo ambaye ni mwanachama wangu katika Kamati ya Kilimo, Uvuvi, Mifugo na Uchumi Samawati. Ni nadra sana Seneta maalum kufanya bidii kiasi hicho kwamba amekuwa ni mmoja wa wale ambao wamewasilisha Miswada muhimu katika Bunge la Seneti. Bi. Spika wa Muda, pamba inatupea takriban Kshs6 bilioni, lakini tuna uwezo wa kupata Kshs7.5 trilioni tukifanya kilimo cha pamba na kuwapa wakulima pembejeo na kuondoa wakiritimba wanaonyanyasa wakulima katika ukuzaji na uuzaji wa pamba. Pamba inakuzwa katika kaunti ishirini na tisa. Kamati ya Kilimo, Uvuvi, Mifugo na Uchumi Samawati iliamua itatembelea wakulima kule mashinani. Tulijua tunapoitisha maoni ya watu, wakiritimba pia watatuma yale mapendekezo yao ili kufanya Miswada inayosaidia wakulima isipite. Tulikaa chini eneo la Kyulu na mji wa Kitui. Tulienda Busia na tukakaa na Seneta Okiya Omtatah na tukapokea maoni kutoka kwa wakulima. Pale Busia, tulipata wakulima kutoka maeneo yote ya Bungoma, Kakamega na Kisumu. Kituo kikubwa cha utafiti wa pamba kiko Kisumu – Makasembo. Jambo ambalo halikufurahisha sana ni kwamba, tulipokuwa tunafanya ushirikishwaji wa umma, zile pesa Kamati ya Kilimo, Uvuvi, Mifugo na Uchumi Samawati inapewa hazikutosha ikabidi, tusiende zaidi. Hata hivyo, tulikuwa tunakusudia kuzuru kaunti zote 29. Bi. Spika wa Muda, hata kama pesa hazitapatikana, tutaendelea kufanya hivyo, kwa sababu ni muhimu kupokea mapendekezo na kuona nyuso zao."
}