GET /api/v0.1/hansard/entries/1242816/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1242816,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1242816/?format=api",
"text_counter": 298,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Kwa hivyo, nikisema Kamati haikuweza kumaliza shughuli zake sababu kulikuwa na upungufu wa fedha, ninamaanisha kwamba, ni lazima tuwezeshwe kama Seneti ili tuweze kufanya kazi kwa makadirio ya bajeti. Naongeza pia kwamba, mambo tunayojadili katika Seneti, si ya siri, ni ya umma. Bi Spika wa Muda, Seneta wa Nandi ametatiza tena mtiririko wa mawazo. Hili ni jambo singetaka kufanya, itabidi nifikirie hata zaidi ili nirudi pale nilikuwa. Katika ukuzaji na uuzaji wa pamba, pamba nyingi kutoka Kenya inauzwa kutoka mataifa ya Tanzania na Uganda. Katika mifumo viwanda vya pamba, wanawake asilimia sitini wanapata faida kwa kupata kazi katika zile kazi. Kuna maeneo ya kiuchumi yanayoitwa Export Processing Zones (EPZ) kwa kimombo. Nguo zingine za kifahari na za bei ghali zaidi kama Polo na Tommy Hilfiger zinatengezewa kwa hayo maeneo ya uchumi, na kisha kuuzwa Canada na kule Marekani halafu Mkenya anazinunua tena kama mtumba. Yeye ndiye mkuzaji wa pamba mkuu ambaye anafaa kufaidika na pesa na zile nguo zinatoka kutoka ukuzaji wa pamba. Wakati Serikali inapanga kupeana pembejeo kama vile madawa na mbolea ya ruzuku, ni vizuri wazingatie kwamba wakulima wa pamba wameachwa pakubwa. Ni jambo la kuhuzunisha kule nimetoka Kirinyaga kwa sababu shamba la kiwanda cha kukuza pamba limeenda. Nilikuja kuuliza Kauli kutoka Kamati ya Mashamba hapa, takriban miezi kadhaa ili tujue kulifanyika nini kwa hilo shamba na kile kiwanda. Kwa sababu ya muda na ninajua kuna wengi wangetaka kushiriki kwa jambo la pamba, mimi pia nikiwa Mwenyekiti, roho na damu yangu huchemka kwa sababu ya kilimo. Ninajua kilimo ndicho kitatunasua kutoka minyororo ya watu tulikuwa tunaita"
}