GET /api/v0.1/hansard/entries/1242884/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1242884,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1242884/?format=api",
"text_counter": 25,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante, Bw. Spika. Pia mimi naungana na wewe kuwakaribisha wanafunzi wa KUSA, kwa kuja katika Bunge letu la Seneti. Jambo muhimu ni kuwa, mtajua taratibu tunazoenenda nazo katika Bunge la Seneti. Kanuni za Kudumu ziko na ndizo zinazoongoza Bunge hili. Bw. Spika, mkiwa hapa hapa mtajifunza mengi. Kuna uhakika ya kwamba wengine wenu wanaweza kuwa Maseneta na mkajikuta hapa. Nina hakika kwamba mnatumia wakati huu kuona viongozi wenu walioko Bunge la Seneti hivi sasa. Pia nyinyi mko na uwezo na taaluma. Mkiendelea katika maisha yenu, hadi itakapotakikana na wananchi kutoka maeneo yenu muwe Maseneta, mnaweza kujipata mahali hapa. Kwa hiyo, karibuni sana. Natumahi mtakaporudi mtakuwa mmejua Bunge la Seneti linafanya kazi gani, ni kina nani wako, na taratibu na Kanuni za Kudumu ziko namna gani. Asanteni."
}